TANGAZO LA MNADA WA MALI ZA SHIRIKA (KWA NJIA YA MAOMBI)

Shirika la Health & Insurance Management Services Organization (HIMSO) linawatangazia wananchi wote mnada wa mali chakavu za shirika (Pikipiki)
1. Orodha ya Pikipiki Zinazouzwa
Pikipiki zinauzwa kama zilivyo
| Aina ya Pikipiki | Namba ya Pikipiki | Maelezo ya Matengenezo Yanayohitajika |
|---|---|---|
HONDA | MC195 BJJ | Inahitaji matengenezo ya Knock Engine, Tyre, na side mirror |
HONDA | MC968 BWG | Inahitaji matengenezo ya Engine, Tyre, Shockup, Side mirror |
HONDA | MC612 CRS | Inahitaji matengenezo ya side mirror, Bulb, gear box, Tyre na Shock up |
2. Masharti na Maelezo ya Kushiriki
Ukaguzi wa Pikipiki: Waombaji wanaruhusiwa kuja kuzikagua pikipiki kabla ya kutuma maombi, kuanzia tarehe 19/05/2026 hadi 26/05/2026
. Gharama za Maombi: Kila ombi litagharimu kiasi cha Tsh 10,000/= (Elfu kumi tu)
. Fedha hii hairudishwi . Uwasilishaji wa Maombi: Waombaji wanatakiwa kuandika barua rasmi ya maombi
kwenda kwa: - HEALTH & INSURANCE MANAGEMENT SERVICES ORGANIZATION (HIMSO)
01 Jacaranda, P.O. Box 2827, 53107 Mbeya, Tanzania Maudhui ya Barua: Barua lazima ionyeshe Namba ya usajili ya pikipiki inayotaka kununuliwa pamoja na Gharama/Bei ambayo mwombaji yuko tayari kununulia
. Njia ya Utumaji: Maombi yatumwe kwa njia ya barua pepe (Email): info@himso.or.tz
3. Maelezo ya Malipo ya Maombi
Fedha za maombi zilipwe kupitia benki ya CRDB
Jina la Akaunti: HIMSO
Namba ya Akaunti: 0150290479807
Kumbuka kuambatanisha ushahidi wa malipo (Bank Slip/Screenshot) kwenye barua yako ya maombi
.
4. Utaratibu kwa Washindi
Washindi watataarifiwa ili waweze kukamilisha malipo ya pikipiki walizoshinda
. Asilimia 50% ya malipo itatakiwa ilipwe papo hapo, na 50% inayobakia ilipwe ndani ya siku kumi na nne (14)
.
5. Mwisho wa Kupokea Maombi
Maombi yote yanatakiwa kuwa yamewasilishwa kabla ya tarehe 29/05/2026, saa 11.00 jioni
Mawasiliano Zaidi
Kwa maswali au ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia:
Barua Pepe: info@himso.or.tz
Simu: 0761 555 552
IMETOLEWA NA: